Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, November 22, 2014

MAMIA WAMUAGA MWANDISHI WA HABARI WA NEW HABARI 2006 LTD, MAREHEMU INOCENT MUNYUKU


Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
  Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI AENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM


 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mbao kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara.

Friday, November 21, 2014

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YAKAGUA MADARAJA LUHEKEI MKOANI RUVUMA.


Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.
Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akitoa maelekezo kwa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.
DSC07428
Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60.

Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikijionea maendeleo ya moja ya madaraja matatu ya Luhekei yanayounganisha wilaya za Mbinga na Nyasa mkoani Ruvuma.

Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

HABARI KUTOKA TFF, MASHINDANO YA TAIFA YA U12 YASOGEZWA


SDL SASA KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 6

AIRTEL YAMWAGA VITABU VYA MILIONI 15 WILAYANI MAKETE –NJOMBE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati), akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton (kulia), utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete. Anaeshudia (kushoto) ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa Shule ya Iwawa, Fadhili Dononda.


Waziri Dk. Mahenge na Meneja wa Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Mushi  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi Wetu
Makete

Mradi wa ‘SHULE YETU’ unaotekelezwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya AIRTEL umeendelea kunufaisha shule kadhaa nchini kwa sasa umeingia wilayani Makete, Mkoani Njombe na kutoa msaada wa Vitabu vya kiada na ziada vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 15 kwa shule tano wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Binilith Mahenge ndiye aliyepokea shehena ya Vitabu hivyo ambapo pamoja na mambo mengine amesifu Msaada huo kuwa unaunga mkono Juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kufanya mabadiliko makubwa katika sayansi na teknolojia nchini kwa kuwekeza kwenye elimu.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe kwa niaba ya shule zingine zinazofaidika na mradi huo zikiwemo  Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete.

Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Mushi alisema "Kampuni ya Airtel tunakabidhi vitabu vya masomo ya KEMIA, FIZIKIA na HESABU ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha wanafunzi kupenda zaidi masomo ya mchepuo wa sayansi ambapo vyote hivi vinathamani ya shilingi milioni kumi na tano".

Akipokea msaada huo, Dk. Binilith Mahenge ameipongeza Airtel kwa kuungana na Rais Jakaya Kikwete aliyethubutu kufanya mabadiliko kwenye masomo ya sayansi.

Dk. Mahenge alisema "nchi yetu itaendelea endapo tu tutawekeza kwa uhakika katika elimu, mataifa yalioyoendelea leo hii kila kitu kinafanikiwa kuwa kiwango cha elimu cha wananchi wake ni cha hali ya juu".

Kwa upande wao baadhi ya wananfunzi wa shule mwenyeji waliopokea vitabu hivyo kwa niaba ya shule nyingine wameeleza kufurahia kwao kupokea msaada wa vitabu hivyo vitakavyokuwa ni suluhisho la uhaba wa vitabu unavyowakabili wanafunzi wa shule 16 za sekondarii zilizomo wilayani Makete.

"Tunaishukuru sana Airtel sisi wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwawa tutavitumia kwa uangalifu kwa manufaa ya wengi na pia tunawaahidi Airtel na Mheshimiwa Waziri kuwa tutahakikisha tunapata matokeo ya ufaulu mzuri kwa kuvitumia ipaswavyo" alisema Kiranja mkuu wa Shule hiyo.

Airtel imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili kuendeleza Elimu Inchini Tanzania kwa kusaidia shule mbalimbalikali ambapo hadi sasa zaidi ya shule 15000 zimeshapewa vitabu vya kiada kupitia mradi huo.

Thursday, November 20, 2014

WIZARA YA UCHUKUZI YAPOKEA MABEHEWA 50 YA KUBEBEA MAKASHA CHINI YA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN)


Moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha likishushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), leo limepokea mabehewa 50 ya kubebea makasha ambapo mradi huu unatekelezwa chini ya Mpango wa Matokeo makubwa sasa(BRN).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk . Shaaban Mwinjaka(mwenye tai ya blue), akiangalia behewa moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha yalishuhushuwa katika bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuniya reli Tanzania(TRL), Mhandisi Amani Kipalo Kisamfu. Kuwasili kwa mabehewa hayo kutasaidia kupunguza msongamano wa mizigo ya makasha na kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Aman Kipalo Kisamfu, kabla ya kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha katika bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kulia kwa Mhandisi Kipalo Kisamfu ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Alois Matei.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akisisitiza jambo wakati wa kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha, leo katika Bandari ya Dar es Salaam. Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba Menejiment ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuyatunza lakini pia na wananchi wanaokaa pembezoni mwa reli kusaidia Serikali kutunza miundombinu ya reli.(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi).

TASWA YAOMBOLEZA VIFO VYA WANACHAMA WAKE, MUNYUKU NA KARASHANIHabari wadau, kwa masikitiko makubwa nawajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya jeshi Lugalo alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.  
Pia mwandishi mahiri wa zamani wa habari za michezo nchini Innocent Munyuku, naye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Hilo ni pigo kwa waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla, maana wote wameondoka wakati bado mchango wao ukihitajika sana. Taarifa zaidi tutaendelea kupeana kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
19/11/2014

UZUNDUZI NA UHAMASISHAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII(CHF) WILAYANI kILINDI MKOANI TANGA


      

unnamedMeneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mkoa wa
Tanga(NHIF)Ally Mwakababu kulia akimuelezea mikakati ya mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF) Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa kulia kwake
kabla ya kufanya uzinduzi wa Uhamasishaji wa wananchi kujiunga na
Mfuko wa Afya ya Jamii wilayani humo (CHF) zoezi ambalo linaendeshwa
na Meneja huyo na maafisa kutokana makao makuu na mkoani Tanga kwa
muda wa siku kumi.
unnamed1 Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa
akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa
Tanga(NHIF) na watumishi wa Halmashauri hiyo Idara ya Afya ofisini
kwake kabla ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na
mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).
unnamed5Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Kilindi,Daudi Mayeji  akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kabla
ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wilayani humo kulia kwake ni Meneja
wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu kushoto
ni Ofisa wa Mfuko huo kutoka makao makuu Isaya Shekifu.
unnamed6Afisa Uanachama wa Mfuko wa Bima ya
Taifa Mkoa wa Tanga (NHIF) Miraji Swalehe akiwaelimisha waendesha
pikipiki kwenye kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi
juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuweza
kupata matibabu muda wote.
unnamed7Meneja wa Mfuko wa Bima ya
Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu akiwahimiza wananchi wa
Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi umuhimu wa
kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake
uliofanywa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa.
unnamed9Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) tokea ulipoanzishwa wilayani humo akimuonyesha kadi zake Meneja
wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu.
unnamed10Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga,Suleimani
Liwowa akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya
Mkoa wa Tanga(NHIF)Ally Mwakababu  na maafisa wengine wa mfuko huo na
madereva wa pikipiki “Bodaboda”mara baada ya kuwakabidhi kadi zao za
uachama wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
unnamed12 DC Liwowa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Muheza Kata ya Masagalu wilayani humo wakati akiwahamasisha kujiunga
na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake.
Mwisho.

Tuesday, November 18, 2014

Laila Ali 'She Bee Stingin'' BONDIA PEKEE WA KIKE ALIYECHUKUA KIWANGO CHA JUU CHA FEDHA KATIKA WANAMASUMBWI

Laila Ali Curtis Conway Curtis Jr.
Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao
Kwa sasa unakadiriwa pia utajiri wake unafikia kiasi cha dola za kimarekani milioni kumi ambazo ni zaidi ya fedha za kitanzania bilioni 16, ambazo ambazo amezitengeneza kutoka katika mchezo wa masumbwi duniani,

Matangazo ya bihashara, pamoja na kazi ya uwanamitindo 
Kutokana na umaarufu wake katika masumbwi , alijikuta akipata mikataba mbalimbali mikubwa ya matangazo ya biashara  katika makampuni na maduka makubwa Duniani, kama maduka ya kuuza vyakula,nguo na vifaa vya michezo hali iliyompatia nafasi ya kujiongezea kipato chake kwa haraka  leila alianza kujihusisha na masumbwi akiwa na umri wa miaka 15, huku msaada wake mkubwa ukitokea kwa baba yake mzazi ambapo baada ya kuonesha uwezo wake kwa mda mfupi arianza kuingia kwenye mapambano ya kimataifa Baada ya kupata ubingwa huo mwaka 2005 aliweza kutoa ubingwa mwingine unaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la ngumi za wanawake ' IWBF kwa kumtwanga Nikki Eplion kwa K,O ya raundi ya nne katika uzito wa female super middleweight title 

Pamoja na uwezo huo, Wapo baadhi ya mabondia wa kike kama Vonda Ward, Leatitia, Robinson na Ann Wolfe wamekuwa wakilalamika kuwa Leila anawakwepa kwa kupangiwa vibonde na kuhofia kupigwa.

Licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa masumbwi, mitindo na matangazo ya biashara kwenye runinga lakini mara kadhaa amekua akialikwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kwa ajili ya vipindi hali inayomfanya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha 

Baadhi ya vipindi hivyo maarufu ni pamoja na agaeorgr Lpez, Dancing with the Stars, American Gladiators,Celebrity Family. The Early Show

Katika historia ya  maisha yake ya ndoa ,leila amesha olewa mara mbili ambapo kwa mara ya kwanza aliolewa na Johnny Mcclain Agost 27,2000,ambaye walikutana kwenye sharehe ya kuzaliwa baba yake mzazi Mohamed Ali wakati anatimiza umri wa miaka 57.

Kabla ya kuoanaMacClain ndiye aliyekuwa promota wake katika michezo ya ngumi za kulipwa jambo ambalo lilimsaidia kufanya vizuri katika mapambano yake yote ambayo ajapigwa wala kutoa droo ata mpambano mmoja akiwa na alama won 24 (KO 21) + lost 0 (KO 0) + drawn 0 = 24  

Baada ya kuoana mwaka 2000 walikuja kuhachana mwaka 2005. mwaka 2007, leila alifunga ndoa na Curtis Conway , ikiwa ni ndoa yake ya pili . wadadisi wa mambo ya kimapenzi wanaeleza kuwa kilichomfanya kuolewa tena ni kutokana na kuwa na mvuto wa kimapenzi alionao mwana dada huyo maili awapo ulingoni,

Leila amefanikiwa kupata watoto watatu akiwa na McClain ambao ni Leilani,Cameron na Kelton. Baada ya kuolewa tena alipata watoto wawili ambao ni Curtis Muhame Conway Aliyezaliwa mwaka 2008 na Sydney  mwaka 2011

Kwa sasa leila amestafu kucheza mchezo wa masumbwi tangu acheze mchezo wake wa mwisho Tareha 3 -2-2007  na Gwendolyn O'Neil na kufanikiwa kumpiga kwa K,O raundi ya kwanza na kutangazwa kuwa bingwa wa mikata miwili ya WBC female super middleweight title
WIBA Women's International Boxing Association super middleweight title
Ingawa kazi kubwa anayofanya kwa sasa ni kutangaza vipindi mbalimbali kwenye television pamoja na mitindo 
Moja ya mambo ambayo yalishangaza ulimwengu katika fani ya mitindo mwaka 2012 akiwa na mimba ya miezi 9, aliweza kushiriki kikamilifu katika maonesho ya mavadhi aliweza kuonesha umahiri wake kwenye jukwaa kwa kupita akiwa kwenye tamasha la mavazi lililofanyika jijini London Nchini Uingereza Novemba 20, 2012

Amestaafu akiwa na rekodi ya kutopigwa ata mchezo mmoja ambapo alicheza michezo  24 alishinda kwa  KO 21 ambapo mabondia watatu pekee ndio aliwashinda kwa point 
huyo ndio leila Muhamed Ali
kwa mahitaji ya DVD ZAKE KWA AJILI YA KUONA MAPAMBANO YAKE MBALIMBALI LIVE TUWASILIANE KUPITIA


Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao

RIPOTI MAALUMU YA CAG KUHUSU AKAUNTI YA ESCROW YAKABIDHIWA KWA MWENYEKITI WA PAC


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya  CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC Mhe. Zitto Kabwe na Kaimu wake Mh. Deo Filikunjombe,Bungeni mjini Dodoma leo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya  CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC,Mhe. Zitto Kabwe .
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiwa ameshikilia vitambu vilivyo Beba ripoti ya CAG kuhusu akaunti ya ESCROW Kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa PAC Mhe.Zitto Kabwe leo.Picha na Deusdidus Moshi,Globu ya JAmii Kanda ya Kati.

MDAU ASIA KINJENGA HAPATA DIGRII YA ELIMU YA JAMII SOSHIOLOJIA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Asia Kinjenga kulia akiwa na nyuso ya furaha pamoja na mwenzie Felician Francis baada ya kumaliza digrii ya elimu ya jamii katika sosholojia wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni
Asia Kinjenga wa pili kulia akiwa na wahitimu wenzie wa mahafali ya 48 katika chuo kikuu cha Dar es salaam
Asia Kinjenga
Asia Kinjenga akiwa na familia yake


Asia Kinjenga kulia akipongezwa kwa kuvalishwa shada la mauwa na mama yake mzazi Bi, Anchimole Lutengano
wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni ambapo alipata digrii ya elimu ya jamii katika soshiolojia
Asia Kinjenga katikati akiwa na mama yake mzazi Anchimole Lutengano kulia na bibi yake wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni ambapo alipata digrii ya elimu ya jamii katika soshiolojia

Sunday, November 16, 2014

K-VANT GIN YADHAMINI BURUDANI ZA MALAIKA BAND TTC CLUB MWISHONI MWA WIKI

 Meneja wa Kanda ya Pwani wa Kampuni ya Megatrade watengenezaji wa kinywaji cha K-Vant gin, ,Geofrey Mkunde kushoto  akimkabidhi katoni ya kinywaji hicho Vendelin Meela wakati wa tamasha kubwa liliodhaminiwa na kampuni hiyo ambapo Malaika band
 walikuwa wakitoa burudani katika ukumbi wa Ttc club Chang'ombe mwishoni mwa wiki iliyopita kampuni hiyo imekuwa ikidhamini burudani mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia raha wateja wao baada ya kazi za kutwa nzima wengine na maofisa kutoka kampuni hiyo
Mkuu wa mauzo wa Kanda ya Pwani wa Kampuni ya Megatrade watengenezaji wa kinywaji cha K-Vant gin, ,Albert Kingu kushoto  akimkabidhi katoni ya kinywaji hicho Vendelin Meela wakati wa tamasha kubwa liliodhaminiwa na kampuni hiyo ambapo Malaika band
 walikuwa wakitoa burudani katika ukumbi wa Ttc club Chang'ombe mwishoni mwa wiki iliyopita kampuni hiyo imekuwa ikidhamini burudani mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia raha wateja wao baada ya kazi za kutwa nzima wengine na maofisa kutoka kampuni hiyo

MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA AAHIDI KUNG'ARA MISS WORLD


Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu safari ya Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2013 kuelekea katika Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2014) nchini Uingereza.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
  
MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko nchini Uingereza.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka  Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu  mzima.
“Nimejifunza mambo mengi hasa kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
Naye Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
Mashindano ya Urembo ya Dunia yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI KWA MAZUNGUMZO JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana kwa mazungumzo.
Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere, akichangia mada wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana Novemba 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile na Mhariri wake, Jackton Manyerere (kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku Novemba 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Wahariri wa Gazeti la Mwananchi mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku Novemba 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri hao baada ya mazungumzo. Picha na OMR
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...