Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 21, 2010

BALOZI WA UTALII WA NDANI AKABIDHIWA ZAWADI

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania,Aloyce Nzuki akimkabidhi Kompyuta ndogo aina ya Dell,Mrembo Salma Mwakalukwa ambaye ni Balozi wa Utalii wa ndani.katika hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi kwa balozi huyo iliyofanyika mapema asubuhi ya leo katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Utalii jijini Dar.kulia ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii,Geofrey Meena na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga.

picha ya pamoja kati ya wadau wa Bodi ya Utalii na Kamati ya Miss Tanzania,pamoja na Balozi wa Utalii wa ndani.

***************** ***************** ****************

Bodi ya Utalii nchini TTB leo imemkabidhi zawadi zake Domestic Tourism 2010 Salma Mwakalukwa kama mshindi wa taji hilo kutokana na vigezo vilivyowekwa katika kinyang'anyiro cha urembo nchini kilichomalizika mwezi ulioisha.

Leo Mkurugenzi mtendaji wa wa TTB Dr. Aloyce Nzuki kumkabidhi rasmi Balozi wetu wa kukuza Utalii wa ndani zawadi zenye jumla ya thamani ya shilingi 4,000,000/=

Dr. Nzuki amesema "Tutamkabidhi Laptop mpya ya aina ya Dell (Window 7) yenye thamani ya shilingi 1,100,000/= na hundi yenye thamani ya shilingi 2,900,000/=".

Amesema Kama mtakumbuka Bodi ya Utalii (TTB) ikishirikiana na Hifadhi za Taifa Tanzania Align Center(TANAPA) na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ilidhamini shindano hili kwa jumla ya shilingi 122, 000,000/= chini ya kauli mbiu isemayo ‘Utalii wa ndani uanze kwa Mtanzania mwenyewe.

Sehemu ya fedha hizi zilizotolewa zilitumika kugharamia safari ya walimbwende wote 30 kutembelea Hifadhi za Serengeti, Manyara, Bonde la Ngorongoro na kwenye mapango ya Amboni Tanga.

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii iliandaa semina kwa walimbwende hao kuhusu utalii wa ndani pamoja na shindano la kumtafuta Balozi wa Utalii wa Ndani 2010. Semina na uchaguzi wa Balozi wa Utalii wa ndani ilifaifanyika tarehe 06/09/2010 katika hoteli ya Giraffe iliyopo jijini Dar es Salaam.

Katika semina hii mada mbalimbali zilitolewa juu ya maana ya utalii/utalii wa ndani, taasisi zinazosimamia sekta ya utalii nchini, aina za utalii/watalii, faida za utalii/utalii wa ndani na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini, ambapo mwakilishi wa TTB alizungumzia, pamoja na mambo mengine, majukumu ya TTB, mbinu za utangazaji utalii/utalii wa ndani na changamoto zilizopo katika kukuza utalii wa ndani nchini. Pamoja na semina hii walimbwende walipewa majarida yanayoelezea utalii wetu.

Wakati wakitoa mada hizi, walimbendwe waliuliza na kujibu maswali yaliyodhihirisha upeo wa juu wa masuala ya utalii wa ndani nchini. Mambo yaliyojitokeza kwenye majadiliano haya ni pamoja na umuhimu wa kuimarisha miuondombinu, juhudi za TANAPA na NCAA kuhifadhi na kukuza utalii, changamoto za kifedha kwa wananchi na umuhimu kutangaza utalii kwa wananchi wengi zaidi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...