Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 5, 2010

JOKHA KASSIM & ISHA RAMADHANI WAIBUKA NA MPYA, KUZINDUA NOVEMBA 21

*WACHA NIJISHEBEDUWE MKE MWENZANGU UNIJUE.

Mwanamuziki mahiri nchini katika miondoko ya Taarab, Jokha Kassim ‘Queen of Golden Voice’, amekamilisha vibao vyake vinne vipya vinavyokamilisha albam itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne huku akiwashirikisha wanamuziki mahiri katika miondoko hiyo, walionaksh na kunogesha vilivyo albam hiyo.

Albam hiyo itakayobebwa na kibao cha ‘Wacha Nijishebeduwe Mke Mwenzangu Unijue’ kilichotungwa na mtunzi mahiri wa mashahiri ya miondoko hiyo, Amin Salmin Abdul.

Akizungumza na Sufianimafoto mtunzi wa kibao hicho kinachotarajia kuteka hisia za mashabiki wa miondoko hiyo, Amin, alisema kuwa katika albam hiyo pia kutakuwa na vibao kama, Kelele za mlango, uliotungwa na Salum Vuai na kuimbwa na Jokha Kassin, ambao pia muziki umeandaliwa na kwa ushirikiano wake mwenyewe Jokha Kassim na Thabit Abdl.

Alizitaja nyimbo nyingine zinazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na MSG za Nini, ambao shairi lake limeandaliwa nae Amin Salmin Amour na kuimbwa na Jokha Kassim na muziki kunakshiwa nae Thabit Abdul ‘Mtoto wa Ilala’, pamoja na Kinyang’anyiro hukiwezi, ambao pia umeimbwa na Jokha Kassim, uliotungwa na Amin Salmin Amour na muziki kuandaliwa na Thabiti Abdul.

Aidha Amin, alisema kuwa Uzinduzi wa albam hiyo unatarajia kufanyika Novemba 21 katika Ukumbi wa Travertine Magomeni Jijini Dar es Salaam, ambapo pia kutakuwa na shoo za utangulizi kutoka kwa waimbaji mahiri wa miondoko hiyo, Khadija Koppa na Isha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ na kusindikizwa na kundi zima la Jahazi Morden Taarab.

Albam hiyo inatarajia kufanya vizuri katika Jukwaa la muziki wa Taarab na hasa kutokana na mashairi na mirindimo iliyomo katika vibao hivyo ambavyo baadhi yake tayari vimekwishaanza kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio, ambapo pia itaambatana na video zake katika VCD, DVD Audio CD na Kanda za kawaida ‘Tape’ ambavyo vyote vinatarajia kupatikana ukumbini siku ya uzinduzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...