Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 9, 2010

MSONDO WAANZA MAONESHO LEO TCC CHANG'OMBE KESHO MAX


Mafundi mitambo wa bendi ya msondo ngoma wakilekebisha mitambo kabla ya kuaanza shoo kushoto ni Ally Momba na Maulidi KIlinda



BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma imelejea Dar es Salaam baada ya ziara ya maonesho matano katika mikoa ya kusini kuanzia Sept 29 mwaka huu baada ya kukaa muda mrefu bila kutembelea kanda hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema ziara hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuitamulisha albamu yao mpya ya Huna Shukrani.

"Tukiwa huko tulifanya kazi ya kuwapa burudan wapenzi wetu walipata nafasi ya kuona mambo mengi yanayohusu bendi yao kama hayo niliyoyasema.," alisema SUPER D

Alisema walianza ukumbi wa Bwalo la Maendeleo, Kilwa na Hoteli ya Lindi Oktoba mosi ambapo oktoba 2 watakuwa Brantare Hall na oktoba 3 watakuwa katika ukumbi wa Madeko Masasi, Oktoba 4 Nachingwea na 5 watakuwa Nyongoro Hall, Ruangwa.

SUPER D alisema mbali na utambulisho wa albamu hiyo bendi hiyo pia itoa fursa kwa wapenzi wake wa mikao hiyo kusikia vibao vipya vya Dawa ya deni kulipa na Lipi Jema vilivyoibwa na wasanii mahiri akiwamo Edo Sanga. ambapo kwa sasa wamerudi kwa kasi zaidi na hali zaidi ya kuisuka bendi hiyo leo itakuwa katika viwanja vya TTC Chan'gombe ambapo kiingilio ni 2000 na kesho itakuwa ukumbi wa Max Bar Ilala kwa kiingilio cha 500 Dar es salaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...