Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 4, 2010

SERENGETI YAZINDUA KAMPENI YA SAIDIA TAIFA STARS ISHINDE


Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Muhammed Seif Khatib akibandika stika kwenye ramani ya Tanzania kuashiria kuwa kampeni kubwa ya kuhamasisha watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa katika mchezo wake muhimu dhidi ya timu ya timu ya Taifa ya Morocco hapo jumamosi,Oktoba 9 2010 imezinduliwa rasmi.kati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Dada Teddy na Rais wa TFF, Leodga Tenga wakishuhudia tukio hilo mchana huu.

Kutoka kushoto ni Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ Jan Poulsen ,Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Dada Teddy Mapunda,Rais wa TFF Leodga Tenga pamoja na Meneja Bidhaa kampuni ya Bia ya Serengeti Dada Nandi Mwiyombela wakiwa katika picha ya pamoja mchana huu mara baada ya uzinduzi.

Ilikuwa ni shangwe na furaha tuu,wakati kampuni ya bia ya serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa timu ya soka taifa stars na wadau mbalimbali wa soka wakati wa uzinduzi wa kampeni ya saidia taifa stars ishinde katika mechi yake ya kukata na shoka itakayofanyika jumamosu hii
Baadhi ya wacheza wa timu ya Taifa Stars nao walikuwepo kushuhudia uzinduzi huo uliofanyika jijini dar leo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...