Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 7, 2010

TUSKER YADHAMINI MICHUANO YA CHALENJI KWA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 675


Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye wa pili kushoto akipokea Mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 675 kutoka kwa Mkurungenzi Mkuu wa SBL Ajay Mehta kulia ni Caroline Ndungu Mkurugenzi wa Masoko SBL na katikati ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano SBL Teddy Mapunda..

Kampuni ya bia ya serengeti ISBL) kupitiam bia yake ya Tusker imedhamini mashindano ya chalenji kwa jumla ya shilingi miloni 675 za kitanzania kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kugharamia tiketi za ndege kwa timu shiriki na maafisa wa CECAFA pamoja na marefa, malazi, usafiri wa ndani, uratibu, zawadi, ada mbalimbali, usalama, gharama za kutumia uwanja, usajili wa waandishi wa habari na gharama nyinginezo.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 27 Novemba mpaka tarehe 11 Desemba mwaka huu ambapo mashindano hayo yanafanyika hapa nchini kwa mwaka huu.

Mashindano ya CECAFA mwaka huu yatashirikisha timu kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burubdi, Djibouti, Somalia, Ethiopia, Sudan, Tanzania, Zanzibar Eritrea na kwa mara ya kwanza CECAFA imeialika timu ya Ivory Coast kama timu mwalikwa wa mashindano hayo. SBL ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano hayo ya CECAFA 2010 kupitia kinywaji chake cha TUSKER

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...