Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 18, 2010

WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2010 WAANZA KAZI YAO LEO






WAANGALIZI wa masuala ya uchaguzi kutoka nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kimaendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wamevitaka VYAMA na wanasiasa wanao wanaia nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao kuwa washindani badala ya maadui kama ilivyo sasa.



Nchi wanachama wa SADC zimetuma ujumbe wa wawakilishi 60 kutoka mataifa mbalimbali, ili kuja Tanzania kuangalia mwenendo wa shughuli nzima ya uchaguzi na kutoa ripoti ya utekelezaji wa demokrasia, ikiwa ni kuitikia mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete.



Akiongea wakati wa utambulisho rasmi wa ujumbe huo, Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa SADC Dr. Tomaz Salomao alisema katika nchi za Kidemokrasia ushindani kati ya chama na chama haupaswi kuwa wa chuki na uadui bali ushindani wenye lengo moja la kuleta maendeleo kwa wapiga kura.



Alisema katika mazingira ya sasa wanasiasa na vyama vyao wanatakiwa kuwa na uvumilivu wa kisiasa wa kiwango cha juu, huku wakieshimu misingi iliyowekwa na utawala wa sheria.



"Tunajua ni wakati wa joto kwa kila mgombea, lakini hilo lisivuruge heshima dhidi ya utawala wa sheria, vyama vyote vinalengo moja la kuleta maendelo kwa wanachi wao ni lazima wajifunze kuishi kama marafiki wanaoshindana lakini si maadui"


Ujumbe huo ambao unaghalamiwa na michango kutoka mfuko wa SADC, utakuwa nchini kwa kipindi chote kuanzia sasa hadi uchaguzi utakapoisha na kutembelea mikoa yote ya bara na visiwani Zanzibar, ambapo watakuwa wakitoa tathimini na ripoti

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...