Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 1, 2010

WANAMITINDO TANZANIA KUTANGAZA UTALII


Kikundi cha Wanamitindo wa Tanzania 'Models Group' wanatarajia kufanya onyesho la mavazi katika ukumbi wa Via Via Club jijini Arusha 0ktoba 2. Akizungumza leo, Mratibu wa onyesho hilo lililopewa jina la 'Time and Beauty' Angel Justace alisema kuwa lengo la kuandaa onyesho hilo ni Kutangaza umoja wao, kuvumbua vipaji vya vijana wenzao na kutangaza Utalii wa nchi ya Tanzania. Angel Justace alisema kuwa kwa sasa wakati umefika kwa vijana kuungana katika kutangaza utalii wa nchi."Sisi kama vijana hatuna budi kujitoa kwa kuungana na kutangaza Utalii wa nchi yetu, kwani bila kufanya hivyo nchi yetu haiwezi kutambulika na wageni hawawezi kujua nchi yetu ina vivutio gani inavyovutia,"Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wanamitindo kutoka Dar es Salaam na wale wa jijini Arusha huku wakipabwa na mbunifu wa mavazi ya asili Gabriel Mollel Sairiamu.Aliongeza kuwa mbali na mbunifu huyo wa mavazi ya asili Gabriel Mollel Sairiamu pia atakuwepo msanii wa kizazi kipya Hussein Machozi.Onyesho hilo limedhaminiwa na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Conservation-Arusha, Kilimanjaro Express Bus, Mwandago Evestiment,Coco Pazzo, Triple A Radio na Masai Club ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...