Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 10, 2010

ZANTEL YAKABIDHI MAMILIONEA WA 'HAMISI MA SMS' PESA ZAO LEO

Kustoka kushoto ni KIko Maganga,Nixon Haule,Rashidi Mtulia, William Mpinga na George Mtey
washindi wakiesabu pesa tasilimu kulia ni Bw. George Mtey Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Zatel Bw.Wiliam Mpinga na mwezeshaji wa promosheni hiyo Bw. Nixon Haule





KAMPUNI ya Simu ya mkononi ya Zantel imekabidhi mamilionea wa promosheni kabambe ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama 'Hamisi ma SMS' ambayo inawapa fursa wateja wote wa Zantel kuweza kushiriki.

Akizungumza baada ya kukabidhi kwa washindi wa promosheni hiyo Dar es Salaam jana Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bw. William Mpinga alisema promosheni hiyo imepangwa katika siku ,wiki na mwezi.

washindi waliokabidhiwa pesa zao jana ni Rashidi Mtulia ambaye ni fundi selemara mkazi wa Mbagala na George Mtey ambaye ni mmiliki wa garege mkazi wa Sinza C wakizungumza baada yakukabidhiwa washindi hawo walisema awajahamini kama wameshinda mpaka walipo kabidhiwa fedha zao jana.


Bw. Mpinga aliongeza kuwa lengo la promosheni hiyo ni kuinua kipato kwa watanzania na wazidi kuendeleza maisha yao kwani tumeona watanzania wengi wanavyojitahidi kushiriki katika promoshini mbalimbali na wanajishindia zawadi kemkem.

Jinsi ya kushiriki promosheni hiyo unatuma neno HAMISI kwenda namba 15587 na utakatwa kiasi cha sh. 350 na mteja atajishindia zawadi kutokana na pointi ambazo atakuwa amejikusanyia kutokana na kushiriki mara nyingi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...