Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 2, 2014

KINANA AFIKA MAENEO YA PEMBEZONI NKASI, AKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA UBOVU WA BARABARA


 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jana, aliendelea na ziara yake katika mkoa wa Rukwa, kwa kutembelea wananchiwalioko pembezoni mwa mkoa huo, ambapo alifika hadi katika Kata ya Wampembe iliyopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilaya ya Nkasi ilimo kata hiyo.
     Katika safari iliyomchukua zaidi ya saa tisa, Kinana na msafara wake alikumbana na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara kutoka Namanyere hadi kwenye vijiji vya kata hiyo kutona na magari kunasa mara kwa mara kwenye tope na makorogoro kwa kuwa barabara haijapata kufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu.
    Kufuatia kujionea changamoto hiyo, Kinana amewambia wananchi wa vijiji vya Wampembe na Ntemba, kuwa ataishauri serikali kuifanya barabara hiyo iwe chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) badala ya sasa ambapo ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na hivyo kuwa vigumu kupatikana fedha za kutosha kujenga barabara hiyo. 
Pichani Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Wampembe, jana,Aprili Mosi, 2014. Na zinazoendelea ni picha zaidi za ziara hiyo na changamoto hizo alizokumbana nazo kama zilizvyopigwa na Bashir Nkoromo aliyeko kwenye ziara hiyo.
Kinana akizungumza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Wampembe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa
 Wananchi wa Kijiji cha Wampembe wakijimwayamwaya kwenye mkutano wao na Kinana
Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Pamoja naye ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka akimpa maelezo.
 Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Nyuma yake ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka
 Kinana akiwafurahia vijana aliowakuta wakifanya kazi katika kijiji cha Wampembe kilichopo kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi. Vijana hao wanafanyakazi katika sekta ya afya na ujenzi
 Kinana mama, baba na watoto wakimpokea kwa hamasa kubwa Kinana katika kijiji cha Wampembe
 Kinana akizungumza na wananchi saa mbili usiku, baada ya kuzuia msafara wake eneo la  kijiji cha Ntemba kaya ya Kate akitoka Kata ya Wampemba kwenda Sumbawanga mjini
 Wananchi katika kijiji cha Ntemba Kata ya Kate wilayani Nkasi wakimsikiliza Kinana, alipoamua kuzunguza nao baada ya kumzuia njiani akitoka Wapembe kwenda Sumbawanga

CHANGAMOTO ZA BARABARA
 Kinana akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara wake kunasa kwenye pori la akiba la  Nkasi, wakati Kata ya Wampembe
 Kinana akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara wake kunasa kwenye pori la akiba la  Nkasi, wakati akitoka Kata ya Wampembe
 Kinana (kulia) akitazama moja ya gari la msafara wake  ambalo lilinasa porini katika harakati za dereva kujaribu kukwepa  eneo baya kwenye barabara katika pori la akiba la  Nkasi, wakati akienda Kata ya Wampembe
 Kinana akitembea kwa miguu baada ya magari ya msafara wake kukwama katika pori hilo la akiba
 Gari la polisi waliokuwa wakisindikiza msafara wa kinana likisukumwa baada ya kukwama katika barabara ya kutoka Wampemba kwenda Namanyere wilayani Nkasi
 Kinana akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete walipokuwa wakitembea kwa miguu baada ya kushindwa kupita kwa magari katika eneo korofi la barabara

MTI WA NGUVU ZA KIUME
 Waandishi wa habari kwenye msafara wa Kinana akishangaa mti ambao unakarinia kuanguka kutokana na kumegwa vbanzi na watu wanaoamini kwa vibanzi kutoka mti huo ni dawa ya nguvu za kiume. mti huo upo pembeni mwa barabara ambako magari ya msafara wa Kinana yalinasa wakati wa kwenda na kutoka kijiji cha Wampembe.
Jamaa akigema kibanzi kwenye mti huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...