Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 8, 2014

BENKI KUU YA TANZANIA MAONYESHO YA SABASABA

.
CHARLES SAMA(MCHUMI)

ABDULI M.DOLLAH(DERECTORATE OF BANKING)


IAN BEN MOSHI MTEJA ALIYETEMBELEA BANK KUU

PATRIC A.FATA(PRINCIPLE BANK OFFICER OPERATION DEPARTMENT ZANZIBAR BRANCH)

NEMBO YA BENKIKUU

Na Gloria Matola                  

  Benk kuu ya Tanzania(BOT)  imewataka wananchi watembelee katika Maonyesho ya Biashara ya 38 (sabasaba) na kutembelea banda ili kupata uelewa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Wito huo umetolewa na  mchumi wa Benki hiyo Charles Sama alisema kuwa wananchi wanapaswa kujua shughuli zinazofanywa na benkikuu kwa kupitia maonyesho hayo ili kufuta dhana ya upotoshaji uliopo mitaani kuhusiana na noti ya Sh 500 uzi wake una kilevi na inatumiwa na mateja(wavuta unga) ili kupata stimu.
Alisema kauli hiyo si kweli kwakuwa noti hiyo inachakaa kutokana na kuwa na mzunguko mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kusababisha kuchaka upesi,
Alifafanua kuwa pamoja na kuwa na mzunguko mkubwa na kusababisha kuchelewa kurudi kwa wakati benki  utunzaji mbaya wa noti hiyo nao unachangia kusababisha kuwa  kuharibika.
“Tumegundua utunzaji mbovu wa noti ya Sh 500 hivyo na kuamua kutengeneza sarafu ambayo itaingia kwenye mzunguko katika mwaka huu wa fedha,”alisema Sama.
Alifafanua suala la kubadilisha sarafu sio geni kwa Tanzania kwakuwa awali tulianza na senti na zikabadilishwa hivyo wananchi wasiwe na mtazamo tofauti kuhusu ubadilishaji huu.
Alisema uvumi wa Tanzania kuthamini sana fedha za kigeni si wa ukweli kwakuwa dola zinatumika katika maeneo ambayo kuna ushirikiano wa kimataifa.
“Si kweli kuwa matumizi ya dola ndani ya nchi yanapewa kipaumbele huo ni mtazamo finyu,sisi hatuwezi kuthamini fedha za watu wa nje na kuacha za kwetu,”alisema Sama.
Alifafanua matumizi ya fedha za kigeni hutumika katika hoteli za kitalii na maeneo mengine  yanayoingia watali wa kimataifa.ALisema katika shule za ndani hawawezi kutumia dola watu wote wanatumia pesa ya kitanzania.
Aliongeza suala la fedha za kigeni linaongozwa na sheria ya fedha ya mwaka 1992 ambayo inatamka bei ya bidhaa na huduma ziwe katia shilingi ya kitanzania isipokuwa biashara za kigeni na masuala ya kimataifa.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...