Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 20, 2014

KAMPUNI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI SAMSUNG YALENGA KUKUZA UCHUMI WA JIJI LA ARUSHA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Mike Seo akiwahutubia na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ufunguzi rasmi  kituo kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.
 Meneja wa Usambazaji wa Samsung Electronics Tanzania, Bw Sylvester Manyara akitoa maelezo  kwa waandishi wa habari na umma.
 Meneja wa huduma wa Samsung Electronics Tanzania, Bw. Mubarak Mikidad akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari katika hafla ya ufunguzi rasmi  kituo kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania, Bw. Mike Seo akiongea na wateja katika ufunguzi rasmi wa kituo kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Mike Seo na Bw Nawaz Ladha, Mkurugenzi  wa Freedom Electronics, mmoja wa wasambazaji wakuu wa Samsung Electronics Tanzania wakikata utepe kufungua rasmi  kituo kikubwa cha bidhaa za Samsung mjini Arusha.

KAMPUNI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI SAMSUNG YALENGA KUKUZA UCHUMI WA JIJI LA ARUSHA

Arusha, 19 Septemba 2014. Kampuni ya Samsung inazindua rasmi  duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa wateja lililopo barabara ya Sokoine mjini Arusha siku ya leo. Uzinduzi huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki na bidhaa halisi za Samsung. Kituo hiki ni cha kwanza kuzinduliwa mkoani Arusha na kampuni hii yenye idadi kubwa ya watumiaji na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama kampuni kubwa inayoongoza kuwa na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afrika. Mkoa wa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa kwamba kituo cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni kituo kikuu cha safari nchini Tanzania”, haya yamesemwa na Mkurugenzi mkuuwa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo

Mbali na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki, duka hili jipya la Samsung litatoa huduma za ziada kwa wateja wake. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake watakaojisajili na uduma ya e-warranty (dhamana) usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.

Mpango huu utawanufaisha wateja wa Samsung watakaosajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba ya IMEI kwenda 15685. Baada ya kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi kwa kipindi cha miaka miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.

Katika kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni, majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, vifurushi vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa kwaajili ya wanunuzi wa simu aina ya Galaxy Trendlite.

Kwa sasa nchini Tanzania kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa mingine.
Duka hili na kituo chake cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia saa 9.30 asubuhi hadi 5.00 jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi 1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Siku kuu.

 Kuhusu Vifaa vya kielektroniki vya Samsung
Teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu takribani 236,000 katika nchi 79, inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia kuingia kwenye teknolojia mpya na matumizi ya smart phone, luninga, air-conditioner, vifaa vya nyumbani vya kieletroniki, kamera, na vifaa vya maofisini kama kompyuta na printers ambavyo vina teknolojia ya hali ya juu kukidhi mahitaji ya wateja. Kujifunza mengi zaidi, tembelea www.samsung.com na www.facebook.com/SamsungMobileTanzania
Kwa taarifa Zaidi wasiliana na:
James Laidoson – Spearhead Africa Ltd
Simu: 0754 252 256

Email: james@spearheadafrica.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...