Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 8, 2014

BALIMI EXTRA LAGER YATANGAZA RASMI UDHAMINI WA MASHINDANO YA MBIO ZA MITUMBWI KANDA YA ZIWA KWA MWAKA 2014.


Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mbio za Mitumbwi Kanda ya Ziwa, zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” iliyofanyiak Dar es Salaam jana.
*****************************************
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya mbio za mitumbwi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu  wa 2014. Mashindano haya ya “kupiga makasia” yanafanyika kwa mwaka wa kumi na tano sasa na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa hususani wale ambao ni wavuvi. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”. Alisisitiza pia umuhimu wa michezo katika kujenga afya bora.
Edith alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya mitumbwi yatahusisha miji mitano ya kanda ya ziwa kama ratiba inavyoonyesha hapo chini kwa hatua ya awali.
TAREHE
MAHALI/MKOA
UWANJA
18/10/2014
KIGOMA
UFUKWE WA MAGEREZA
01/11/2014
BUKOBA
UFUKWE WA SPICE BEACH
08/11/2014
MWANZA
UFUKWE WA MWALONI
15/11/2014
KISIWA CHA UKEREWE
UFUKWE WA HOTELI YA MONARCH
22/11/2014
MUSOMA
UFUKWE WA BWALO LA POLISI
 Washindi watakaopatikana katika miji hii watashindanishwa kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda linategemewa kufanyika jijini Mwanza mwanzoni mwa mwezi December. Tarehe 6 Disemba 2014.
Edith Bebwa akizungumzia zawadi za mwaka huu alisema kwamba katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na nne kama zawadi za pesa taslimu kwa washindi. Mpangilio wa zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini; 
ZAWADI
NGAZI YA MKOA
WANAUME
NGAZI YA MKOA
WANAWAKE
NGAZI YA KANDA
WANAUME
NGAZI YA KANDA
WANAWAKE
Mshindi wa Kwanza
900,000
700,000
2,700,000
2,300,000
Mshindi wa Pili
700,000
600,000
2,300,000
1,700,000
Mshindi wa Tatu
500,000
400,000
1,700,000
900,000
Mshindi wa Nne
400,000
300,000
900,000
700,000
Mshindi wa 5 - 10
6 @ 250,000
6 @ 200,000
6 @ 400,000
6 @ 250,000
Edith alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi katika miji iliyotajwa ili kufurahi kwa pamoja katika matamasha haya. Alisisitiza wasisahau mila na tamaduni zao katika kipindi ambacho watu wengi hupenda kuiga tamaduni za kimagharibi. Alimaliza kwa kuwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra Lager inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na;
Arthur Kanza, Balimi Extra Lager Brand  Manager, simu; +255 767 266 717,
Kuhusu TBL;
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.
Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.
Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.
Kuhusu SABMiller;
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India. SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...