Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, December 14, 2014

NYONI AMBWAGA CANNAVARO TUZO ZA TASWA, MOTTO AFANYA MAAJABU


Beki wa Azam FC, Erasto Nyoni (kushoto), akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2014, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Asah Mwambene muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hizo zlizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ndani ya Ukumbi wa Diamond Jublee. Mgeni rasmi katika tuzo za Twaswa 2014, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein (kulia), akikabidhi tuzo ya mchezaji wa jumla Sheridah Boniface ndani ya Ukumbi Diamond Jublee usiku wa kuamkia leo.Mama Fatuma Karume akikabidhiwa tuzo ya Heshima na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohame Shein.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecky Sadiki (kushoto), akikabidhi tuzo ya Ngumi za kulipwa kwa  Francis Cheka mara baada ya kutangazwa mshindi ndani ya Ukumbi wa Diamond Jublee.Waziri wa Vijana Habari,Utamaduni na Michezo Fenela Mkandala (kushoto),akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Gofu Wanaume Ridhaa  iliyochukuliwa na Nuru Mollel.Mgeni rasmi wa tuzo hizo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein akizungumza jambo kabla ya kuhitimisha kwa zoezi la utoaji tuzo hizo.Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tuzo mbalimbali zilizokuwa zikitolewa usiku huo ndani ya Ukumbi wa Diamond Jublee.
KIRAKA wa klabu ya Azam  na timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Erasto Nyoni usiku wa kuamkia leo, alimbwaga nahodha na beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika tuzo za mwaka 2013/14 katika kipengele cha mchezaji bora wa soka wa kitaifa.
Katika tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), zilifanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar na Nyoni kufanikiwa kuitwaa kwa kuwagaragaza Cannavaro na straika wa Simba, Elias Maguli ambao walifanikiwa kuingia hatua ya fainali.
Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, nyota wa Azam, Muavori Coast, Kipre Herman Tchetche aliwabwaga Mrundi, Amisi Tambwe wa Simba na beki wa Yanga,     Mnyarwanda, Mbutu Twite.
Mbali na tuzo hizo, shujaa katika tuzo hizo alikuwa ni straika yosso wa timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, Sheridah Boniface ambaye alitwaa tuzo tatu mfululizo ikiwa ni rekodi ya aina yake tangu tuzo hizo zianzishwe mwaka 2006.
Sheridah ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya Afrika ya wanawake ya Airtel Rising Stars iliyofanyika nchini Nigeria, usiku wa jana aling’ara kwa kutwaa tuzo ya Wanamichezo chipukizi akiwangusha Omary Sulle (tenisi) pamoja na kipa wa Azam, Aishi Manula.
Kinda huyo mwenye miaka 17, aliibuka tena kidedea kwenye tuzo ya mchezaji bora wa wanawake akiwazima Sophia Mwasikili na Amina Ally huku pia akitwaa tuzo ya jumla.
Wachezaji wanaocheza nje ya nchi, Mbwana Samatta anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo aliondoka na heshima hiyo kwa ‘kuwakalisha’, Thomas Ulimwengu ambaye wapo timu moja pamoja na mwendesha baiskeli Richard Laizer aliye Afrika Kusini.
Tuzo nyingine ni: Francis Cheka (Ngumi za kulipwa),  Seleman Kidunda (ngumi za ridhaa).
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...